Burudani

New Music: Kus Ma wa Camp Mulla aiboresha Rock n Roll ya (1950) kuwa hip hop ya (2013) katika “TUTTI FRUITTI” (Audio)

Miezi michache iliyopita kundi la Camp Mulla lilizindua solo projects za wasanii wake na safari hii producer wa kundi hilo Kus Ma amedondosha dini lake binafsi, ni wimbo flani uliofanyiwa utundu kwa kufanyiwa sampling ya wimbo wa miaka ya 50.

KUS MA

Je wewe ni mfuatiliaji wa muziki wa Rock n Roll? Kwa wale kizazi cha Diamond na Young Killer nategemea jibu la NO! Anyway let me get straight to the point…Kus Ma ame sample wimbo wa mwaka (1957) wa miondoko ya Rock n Roll wa mwanamuziki aitwaye Little Richard, lakini ameamua pale mwanzo kukiweka kipande cha wimbo alio sample ili kusaidia hata asiyeujua afahamu alipoitoa, kisha akaichanganya na midundo ya kisasa na kama unavyojua Camp Mulla huwa hawakosei hasa katika production zao.

“Tutti Fruitti” ndio jina la wimbo wa mwanamuziki mkongwe Little Richard (mwenye miaka 80 sasa) ambao Kus Ma ameurudia kisasa zaidi katika miondoko ya hip hop kwa jina hilo hilo “Tutti Fruitti” akimshirikisha member mwenzake wa Camp Mulla Shappa Man.

Isikilize hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents