Michezo

Newcastle United kupigwa mnada

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Newcastle United, Chris Waddle amesema kuwa anamsikitikia, Mike Ashley kwa maamuzi yake ya kuiweka sokoni timu hiyo.

Mmiliki wa klabu ya Newcastle United, Mike Ashley (kushoto mwenye shati jeupe)

Bosi wa timu hiyo, Mike Ashley ambaye anaimiliki kwa zaidi ya miaka 10 sasa amekuwa chanzo cha mgawanyiko wa Newcastle United tangu alipoichukua mwaka 2007 amesema mchezaji huyo, Waddle.

Taarifa zinaeleza kuwa bosi huyo hana mahusiano mazuri na wapenzi wa klabu hiyo wala hayupo karibu na vyombo vya habari katika kuzungumzia matatizo ya timu hiyo.

Timu ya Newcastle imefamikiwa kumaliza nusu ya ligi kuu nchini Uingereza mara mbili pekee tangu klabu hiyo inunuliwe na Ashley kwa dau la paundi milioni 134.4 Julai mwaka 2007.

Ikiwa chini ya Alan Pardew msimu wa mwaka 2011/12 timu hiyo ilimaliza katika nafasi tano za juu na kwa mara ya mwisho ilimaliza katika nafasi za juu ilikuwa msimu wa mwaka 2003/04 na kufanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Europa League.

Licha ya mashabiki kuhitaji kushiriki katika michuano mikubwa lakini, Mike Ashley  mwenye umri wa miaka 53 ameona kuwa hawezi kuwekeza fedha ambazo zitaweza kushindana na klabu za  Chelsea, Manchester United, Arsenal na Manchester City kwakutambua kuwa hana fedha za kutosha.

Newcastle sasa inahitaji muwekezaji mwenye uwezo wa kutosha

Rekodi za klabu ya Newcastle ikiwa chini ya mmiliki wake wa sasa Mike Ashley

Ashley kwa mara ya kwanza alitangaza kuiweka sokoni klabu hiyo mnamo Septemba mwaka 2008 na kusababisha maandamano kwa mashabiki kwa kufuatia kuondoka kocha, Kevin Keegan.

Kisha mwezi Desemba mwaka huo huo akaitoa sokoni na mwaka uliyofuata 2009 mwezi  May alitangaza kuiuza tena.

Hapo jana siku ya Jumatatu imetoka habari ya kuuzwa tena huku mmiliki wa klabu hiyo, Ashley akiwa na matumaini ya kumalizika kwa biashara hiyo kipindi cha  Christmas.

Miaka 10  ya Ashley akiwa mmiliki mpya wa Newcastle, makocha 10 ameajiri katika kipindi chake.

Katika dimba la nyumbani la St James’ Park limekuwa sio sehemu salama kwa makocha tangu Mike Ashley aimiliki timu hiyo.

Ni kocha Rafael Benitez pekee ambaye ameonekana kukaa kwa muda mrefu pengine kuliko wengine waliyomtangulia ambapo amecheza jumla ya michezo  64 akiwa kama meneja.

Miaka 10 ya Ashley akiwa mmiliki mpya wa Newcastle, ameshinda michezo minne pekeee ya FA Cup bila ubingwa.

Iliwahi kuripotiwa kuwa Ashley aliwahi kutangaza dau nono la paundi milioni 20 kwa kikosi chake endapo watachukuwa ubingwa wa FA CUP lakini vijana hao wakahitaji kuhakikishiwa kama bosi huyo mwenye miaka 10 ndani ya klabu hiyo atatoa mzigo huo.

Newcastleimeshinda michezo minne pekee ya FA Cup katika misimu 10 huku ikishindwa kuingia hata katika duru la nne la michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents