Michezo

Ni Man City Tu wenye uwezo wa kuizuia Liver ‘Becoming Invicible’, mambo matatu ya kuangazia Premier League

Hakika wikiend hii iliyopita mashabiki wa soka waliweza kuona wababe wa Premier League Liverpool wakimshikisha adabu kocha machachari na mwenye maneno mengi zaidi ‘The Special One’ Mreno, Jose Mourinho akiwa na kikosi cha Tottenham.

Liverpool overcame another major hurdle in their title challenge as they won 1-0 at Tottenham

Kama ilivyo kawaida yao vijana wa Klopp walishuka dimbani na kuondoka na pointi tatu walizo agizwa na mashabiki wao bila kujali ukali wa Mourinho, wakamchapa bao 1 – 0 tu na kufanya kuonesha kuwa wao kwa sasa wameshindikana na itahitaji muda mrefu pengine kupata mpinzani wa kuwatisha ukiachana na Manchester City ambao kidogo wamekuwa wakitoana jasho.

1) Liverpool inaunyemelea ubingwa kwa fujo zote bila kujali heshima na ukubwa wa timu nyingine Premier League.

Jurgen Klopp amekuwa mtu wa kutembeza kichapo tu katika kila timu anayo kutana nayo mbele na kuzidi kujiwekea rekodi.

Mashabiki wengi wa soka waliamini Klopp sasa amekutana na kisi cha mpingo kwa Mreno, Jose Mourinho akiwa nyumbani kwake lakini kumbe zama zimebadilika sana pengine hakuna Mkate mgumu mbele ya Chai na pengine wanasoka wameshindwa kwendana na muda baada ya kuona Tottenham akizibwa mdomo kwa bao 1 – 0 wakati majogoo hao wakiwa katika mbio za Ubingwa.

Liverpool sasa inakuwa klabu yenye mwanzo mzuri wa msimu kuliko timu yoyote ambazo zinapatikana kwenye ligi tano kubwa Barani Ulaya.

Inalazimika sasa wapenzi wa soka kwendana na kasi ya Liverpool maana hakuna namna, wamecheza michezo 21 wakiwa na jumla ya pointi 61 (ushindi mechi 20 , sare 1 na kufungwa 0) kwanini usiamini kuwa hawa vijana wa Klopp wapo kwenye sayari nyingine.

Sergio Aguero with the matchball after a record-setting hat-trick in City's thrashing of Villa

2) Manchester City watakuwa na kibarua kizito cha kupata mbadala wa Aguero

Mwezi uliyopita Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisikika akisema kuwa kutakuwa na kazi kubwa sana ya kupata mbadala wa Muargentine, Sergio Aguero atakapohitaji kuondoka pale mkataba wake utakapofikia mwisho 2021.

Hilo wala halina ubishi mara baada ya Aguero kufanya yake siku ya Jumapili kwa kuonyesha uwezo mkubwa sana kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.

Aguero alifunga hat-tricks yake ya (12) suki huo ambao walishinda kwa jumla ya mabao 6 – 1, mbali na mabao hayo matatu alifanikiwa kuandika historia yake na kuvunja ile iliyowekwa na Henry.

Sasa amekuwa mchezaji wa kigeni ambaye sio Muingereza mwenye mabao mengi zaidi kwa kufisha magoli 177 dhidi ya 175 alifunga legend wa Arsenal, Mfaransa Thierry Henry.

Reece James applauds the Chelsea fans after Saturday's 3-0 home win over Burnley

3 ) Chelsea huwenda sasa wamepata kile walichohitaji

Mdogo mdogo ndiyo mwendo, Frank Lampard amezidi kuendelea kuimarisha kikosi cha Chelsea na pengine yeye ndiye kocha yule waliyekuwa wakimuhitaji kwa kipindi chote.

Katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi umekuwa mzuri kwa upande wao na kuongeza murali kwa wachezaji na benchi zima la ufundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents