Burudani

Nikki wa Pili ashusha ‘nondo’ kwa vijana

Rapper Nikki wa Pili kutoka kutoka kundi la Weusi amewataka vijana kujitengezea mfumo binafsi wa kujikwamua katika changomoto zinazowakabili.

Kupitia mtandao wa Instagram Nikki ameeleza kuwa ni vema vijana kuepuka mifumo ambayo haitawezesha ndoto zao kutimia bali wajaribu kufanya vyao hata ikiwa katika hatua ya chini.

“Kwa kijana uliyezaliwa Tanzania tambua kuna utamaduni mkubwa wa kuwapangia vijana cha kufanya, kusema, kuvaa, hata huko mashuleni au vyuoni sauti za vijana au wanafunzi hazina nafasi katika kuandaa mitaala wala namna ya kuendesha vyuo au shule kila kitu kinapangwa na walio wakubwa zaidi ndio mana kufanikiwa wengi wanaanza juu ya miaka 38,” ameandika Nikki.

“Kuna mifumo mingi ya kuwafelisha vijana, msifuate mifumo au mitizami isiyo akisi ujana wenu nguvu yenu na ndoto zenu, msisubiri vitoke juu kwa wakubwa kama msaada, anzieni chini jifunzeni kupitia nyie kwa nyie. Niamini mimi hata kwenye madarasa ya masters hakuna uhusishwaji wa sauti za wanafunzi katika lolote wewe lipa ada ingia darasani fundishwa pita hivi,” amesisitizi.

Nikki wa Pili kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Quality Time’ ambayo pia ni funzo kwa vijana katika kuzingatia muda ambao wanapaswa kuutumia kwa kufanya mambo yenye manufaa kwao.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents