Michezo

Nilisita kuingia mkataba mpya na Arsenal – Wenger

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa alisita kuingia mkataba mpya na klabu hiyo akihofia kuiyongoza kwa mara nyingine tena.

Wenger aliingia mkataba wa miaka miwili na Arsenal mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Akihojiwa na kituo cha runinga cha Ufaransa cha Telefoot kocha huyo mwenye historia kubwa na Arsenal amesea kuwa hofu yake ilichagizwa na mambo yake binafsi.

Wenger ameiyongoza klabu hiyo tangu mwaka 1996 huku ikishindwa kuwepo ndani ya nne bora wa simamo wa ligi ya Uingereza msimu uliyopita na kuwa mara ya kwanza kwa kocha huyo.

Arsenal walianza michuano ya msimu huu ya ligi ya Uingereza kwa kuwafunga Leicester 4-3 kabla kupoteza kwa Stoke kwa goli 1-0 na Liverpool 4-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents