Michezo

Nimekuja Simba SC kusoma sikuja kufanya maajabu  –  Irambona Juma (Video)

Baada ya Klabu ya soka ya Simba hii leo kumtambulisha rasmi kocha msaidizi, Irambona Masud Juma kuchukua mikoba iliyoachwa na Jackson Mayanja mwalimu huyo amesema yeye anasura mbili ya upole na ukali hivyo atazitumia zote hizo katika kuhakikisha wachezaji wanailetea manufaa timu hiyo.

Kocha huyo msaidizi ameyasema hayo mara baada ya kupata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari.

“Si unaona mkono una sehemu ya mbele na nyuma, hii ya mbele inaonyesha mimi nimpole sana  na huku nyuma inaniwakilisha ukali lakini natumia pande zote mbili si unajua ukiwa kocha unajaribu kushirikiana nakuelekezana sisisote tunatafuta pesa sasa mchezaji lazima atafute riziki yake na ushindi pia siwezi kukubali kuona mtu ananiaribia kazi yangu.” Amesema Irambona Juma

Juma ameongeza  “Mimi kuwa mwalimu msaidizi ndiyo maisha yalivyo kunasehemu unaanzia na kisha unafika hatua fulani unapanda kule Rwanda nilisema sitaki kuwa msaidizi licha ya kuwa mwaka huu kuwa kocha bora ila nimeamua kuja Simba kusoma kwakuwa hii ni timu kubwa nahitaji jina langu lisogee mbele. “Sisi ni binadamu huwezi kutoa ahadi kwa mtu kwakuwa aliejuu ni Mungu lakini tunamuombayeye tufike mbali tu bali tupate zaidi huu mwaka.”

Kocha, Juma atasaidiana na Omog katika kipindi hiki ambacho timu hiyo inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya mahasimu wao klabu ya Yanga Octoba 28 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents