Michezo

Okwi atua Singida kuifuata Mbao FC Mwanza

Mara baada ya ushindi mnono waliyoupata hapo jana wa jumla ya mabao 3-0 kikosi cha timu ya soka ya Simba hivi sasa kipo safarini kikiwa na mchezaji wake raia wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi kuelekea Mwanza kujiandaa na mchezo wake dhidi ya timu ya Mbao FC  ambapo kwa hivi sasa kimefika Singida mjini.

Simba SC inaifuata Mbao FC katika mchezo wa duru ya nne ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 21 ya mwezi huu huku ikiwa na rekodi nzuri msimu huu ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Mwenyeji wa mchezo huo klabu ya Mbao FC itaingia uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu ya kukubali kipigo kutoka kwa Mtibwa Sugar cha mabao 2-1 walipokutana Manungu mkoani Morogoro katika duru ya tatu ya Ligi hiyo wikiendi hii.

Matokeo Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa tatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents