Michezo

Olivier Giroud kuikosa Ujerumani

Shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) limesema kuwa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud atakosa mchezo wa kirafiki baina ya timu yake ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne kufuatia majeraha yanayomkabili kwa sasa na hivyo kurejea The Gunners kwaajili ya matibabu.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Olivier Giroud

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alifunga bao lake la 29 katika timu yake ya taifa wakati Ufaransa ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wales siku ya Ijumaa kisha kufanyiwa mabadiliko 73 kufuatia majeraha aliyopata.

Giroud ambaye ameifungia Arsenal jumla ya mabao matatu msimu huu huenda akaikosa derby ya London Kaskazini baina ya klabu yake dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya Jumamosi.

Meneja wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps huwenda akatafuta mbadala wa mchezaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents