Oscar dos Santos aanza kuwasha moto ndani ya Shangai SIPG

Mchezaji wa Shangai SIPG, Oscar dos Santos aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea klabu ya Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 ameanza kuuwasha moto ndani ya timu hiyo.


Oscar akiwa amevaa jezi ya Shaghai SIPG katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Batin in Doha

Oscar ambaye ni mchezaji wa pili kulipwa mshahara mkubwa duniani baada ya Carlos Tevez amefanikiwa kufunga goli lake la kwanza akiwa na timu hiyo ya China ilipocheza alfajiri ya Jumatatu hii katika mechi ya kirafiki dhidi ya Al Batin in Doha ya Qatar.

Baada ya mchezo huo, Oscar alionyesha furaha yake alipozungumza na waandishi wa habari na kusema amefanya mazoezi na timu hiyo kwa muda wa siku mbili pekee lakini amefurahi kuona goli lake ndio limeipatia timu yake ushindi kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

“I only trained for two days and this is my first game. This is the start of a new season and we had only one goal, which was to win the game,” amesema mchezaji huyo. “My team-mates played very well today. The Chinese guys tried to help us integrate. It’s difficult to have a good game in such a short time but they made it happen,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW