Burudani

Watu 16 wakamatwa kwa kumpora Kim Kardashian

Watu 16 wamekamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa kutumia nguvu uliomkumba msanii Kim Kardashian West mjini Paris mwezi Oktoba.

Utawala unasema kuwa msanii huyo raia wa Marekani aliporwa kwa nguvu na takriban watu wawili waliokuwa wamevaa sare za polisi.

Wanaume hao waliingia chumba cha kifahari alichokuwa Kim Kardashiana kabla ya kumfunga na kumfungia kweye bafu.

Kisha wanaume hao walitoroka na vito vya thamani ya dola milioni 10.5.

Polisi wa Ufaransa wanasema kuwa uchunguzi wa DNA ndio ulichangia kukamatwa kwa watu hao.

Wanaume hao waliakamatwa wakati wa uvamizi ulioendeshwa maeneo ya Paris, Normandy na la Frech Riviera kufutia uchunguzi wa miezi kadha.

Moja ya uchunguzi wa DNA ulikuwa sawa na ule wa mtu anayejulikana kwa polisi kuwa mhalifu.

Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West alisema alikuwa na hofu kuwa angeuawa wakati huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents