Habari

Pakistan: Watu wenye silaha waishambulia hoteli ya kifahari

Wanaume wapatao watatu wenye silaha wamevaimia hoteli ya kifahari huko Gwadar katika jimbo la Balochistan, utawala wa nchi hiyo umeeleza.

Image result for Pakistan Gwadar attack

Vikosi vya usalama vimelizunguka eneo la hoteli hiyo ya ‘ Pearl Continental’ katika mji wa Gwadar baada ya shambulio lililofanywa na watu watatu wenye silaha. Gazeti la Dawm limeripoti.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Milio ya risasi ikiwa inaendelea kusikika kutokea ndani ya hoteli. Ripoti kamili inayoeleza idadi ya wageni waliokolewa bado haijatoka.

Mji huo ambao ni kituo cha mabilionea wa uwekezaji wa miradi kutoka China.

Gwadar is the centrepiece of a multi-billion dollar Chinese infrastructure project in Pakistan [File: Caren Firouz/Reuters]

Aidha hoteli hiyo inatajwa kuwa na wageni wengi kutoka nje ya nchi ambao ni watalii na wafanyabiashara, lakini bado haijajulikana ni wangapi walikuwa katika hoteli hiyo.

Mashambulio ya aina hiyo ni mengi katika jimbo la Balochistan, eneo ambalo ni la watu maskini zaidi katika nchi hiyo ya Pakistani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents