Michezo

Pambano la mabondia Cheka na Maugo laiva…Cheka ahidi kuweka heshima kwa Wamakonde


Kitwe General Traders wameeleza kuwa maandalizi ya pambano la ngumi kuwania ubingwa wa I.B.F Intercontinental East Africa yamekamilika. Mkurugenzi wa kampuni hiyo promota Lucas Rutainurwa alisema anayo furaha kuutambulisha mkanda rasmi ambao utashindaniwa na mabondia Francis Cheka wa Morogoro dhidi ya Mada Maugo wa Lorya Mara ambao ulikuwa umewasili jijini Dar-Es-Salaam kutoka nchini Marekani.

Promota huyo alimtambulisha bwana Moses V Katabaro ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Akai Agent ambao pia ni wadhamini wa pambano hilo ambao nao kupitia mkurugenzi huyo walithibitisha kutoa gari kama zawadi kwa mabondia hao wawili na kwamba ameshalikabidhi gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 8 wiki iliyopita.

Naye Bondia Rashid Matumla ambaye atakuwa kamishana wa mpambano huo alisema pambano hilo litafanyika tarehe 28 mwezi ujao katika ukumbi wa PTA sabasaba a kwamba anayo furaha kubwa kuteuliwa kuwa Kamishana wa kanda kimkoa wa Dar-Es-Salaam.

Bwana Matumla alienda mbali na kusema katika pambano hilo kutakuwa na mampambano mengine kama pambano la mabondia wa kike kati ya Asha Ngedere dhidi ya Salima Kihombwa na mapambano mengine ni kati ya Seba Temba dhidi ya Venasi mponji, Sadiki Momba dhidi ya Cosmas Cheka, Yohana Robert dhidi ya Said Dimoso na pambano kati ya Nasibu Ramadhani dhidi ya Moro Best.

Akiongea na waandishi wa habari bondia Mada Maugo alisema kwa sasa hana wasi na kuutwaa mkanda huo kwani anaimani waamuzi wa nje watathibitisha ubora wake hivyo anatarajia kuanza mazoezi tarehe 5 mwezi wa nne.

Naye Francis Cheka alisema kwa upande wake hana wasiwasi wowote na pambano hilo kwani suala la kuuchukua mkanda huo sio ishu kubwa kwake kwani Mada Maugo sio saizi yake kwani anachowaza sasa ni kuvunja rekodi za Rashidi Matumla na kujiongezea mataji mengi zaidi na wala hasumbuki na tamba za Maugo. Pia alichukua nafasi hiyo kuwaambia wamakonde ambao yeye anasema ni mwenzao kwamba siku hiyo ataweka heshima kwa kutwaa mkanda huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents