Picha

Papa adai ana mashaka kama Donald Trump ni mkristo, naye ajibu mapigo

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amedai ana wasiwasi kama Donald Trump ni mkristo kama anavyodai.

021816-trump-pope-getty-tmz-6

Japo hakumtaja kwa jina, kauli ya Papa isemayo, “Mtu anayefikiria tu kujenga kuta, popote walipo na sio kujenga madaraja, sio mkristo.”

Inaonekana kuwa hilo lilikuwa dongo kwa Trump anayewania urais wa Marekani mwaka huu na anayetaka kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Trump amejibu mapigo kwa kudai: Kwa kiongozi wa kidini kuhoji imani ya mtu ni jambo la aibu. Mimi ni mkristo ninayejivunia.”

Trump anaamini kuwa viongozi wa Mexico waliokutana na Papa wamemuambia uongo kuhusu mambo ya uhamiaji.”

“Siku Vatican inashambuliwa an ISIS, kitu ambacho kila mtu anajua kuwa utakuwa ushindi mkuu kwa ISIS, naweza kuahidi kuwa papa atatamani na kuomba kuwa Donald Trump angekuwa rais sababu hicho kisingetoke,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents