Burudani

Picha: Davido ampatia baba yake gari la 395m kwenye birthday yake

Jumapili hii ilikuwa ni siku muhimu kwa baba yake Davido, Adedeji Adeleke ambaye ametimiza miaka 60 ya kuzaliwa. Katika kusherehekea hilo Davido alimpatia baba yake zawadi yenye thamani ya zaidi milioni 395 kwa fedha za Bongo.

Hitmaker huyo wa If, alimpatia baba yake gari aina ya Bentley lenye thamani hiyo kama zawadi kwenye sherehe hiyo ambayo ilifanyika Atlanta. Wakati huo huo Davido amethibitisha kupitia mtandao wa Instagram kuwa baba yake siyo wamchezo mchezo kwa kuwa akaunti yake inasoma kiasi cha bilioni 30 kwa fedha za Nigeria.

Kupitia mtandao huo, muimbaji huyo ameandika, “HAPPY 60TH BIRTHDAY DADDY!!!! YOU ARE TOO BLESSED DADDY !!! 30 BILLION FOR D ACCOUNT FOR REAL NO BE MOUTH !! ????.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents