Habari

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mjukuu wake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha Hubasha Ngasa (62) mkazi wa Kijiji cha Ngonho baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka minne.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili 24 mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda shambani kulima.

Ukongoji alisema, “Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea, walikuta tayari mshtakiwa amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri.”

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents