Michezo

Picha: Iniesta atua ligi ya Japan

Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta amejiunga rasmi na klabu ya Vissel Kobe inayoshiriki ligi kuu ya nchini Japan.


Andres Iniesta akiwa na mmliki wa Vissel Kobe, Bilionea Hiroshi Mikitani ambaye pia ni CEO wa wadhamini wakuu wa Barcelona, Rakuten.

Iniesta amesaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea timu hiyo.

Kiungo huyo ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari na mmliki wa Vissel Kobe, Bilionea Hiroshi Mikitani ambaye pia ni CEO wa wadhamini wakuu wa Barcelona, Rakuten.

April 27 ya mwaka huu, Iniesta alitangaza rasmi kuondoka Barca baada ya kuicheza timu hiyo kwa miaka 22 na kushinda vikombe 31.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents