Habari

Picha: Maandamano ya Venezuela yaendelea kushika kasi

Moto unazidi kumwakia Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro kwani Maandamano ya kumpinga rais huyo yameendelea tena kwenye siku ya wafanyakazi duniani, huku yakiwa yametimiza mwezi mmoja tangu yalipoanza.

Katika hali ya kuwashangaza wengi, Rais Maduro, wakati akihutubia siku ya mei mosi, alitoa wito wa kuundwa kwa Bunge la katiba nchini humo, ambalo litakuwa na mamlaka ya kuandika katiba mpya. “Ni lazima kurekebisha hali hii, hasa Bunge mbovu lililopo sasa,” amesema Maduro katika hotuba hiyo.

Bunge la kitaifa limekuwa likitaka Rais Maduro ajiuzulu, wakati taifa hilo likikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents