Michezo

Picha: Mapokezi ya bingwa wa Australia Open, Roger Federer yafana Switzerland

Mchezaji tennis raia wa Switzerland, Roger Federer amepata mapokezi makubwa baada ya kuwasili nchini kwao na taji lake la 20 la Grand Slam la Australian Open alilolitwaa siku ya Jumapili.

Mashabiki mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa ndege wa Kloten huko Zurich siku ya Jumanne wakisubiria ujio wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 akiwa na taji lake.

Federer amemshinda Marin Cilic  kwa jumla ya seti 6-2, 6-7, 6-3, 3-6, 6-1, huko Melbourne.

Kwa ushindi huo unamfanya Mswizi huyo kujiunga na mastaa wengine kama Serena Williams, Margaret Court na Steffi Graf kutwaa mataji 20.

 

Picha zikimuonesha Staa huyo wa mchezo wa Tennis akiwasili nchini kwao Switzerland

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents