Michezo

Picha: MO aongoza kikao cha bodi ya wakurugenzi klabu ya Simba kwa mara ya kwanza  

Mfadhili mkuu wa klabu ya Simba na mfanya biashara, Mohammed Dewji hapo jana Novemba 10, 2018 siku ya Jumamosi amefanya kikao cha kwanza cha bodi ya wakurugenzi.

Dewji amefanya kikao hicho akiwa wajumbe wa bodi hiyo ambao walichaguliwa katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba uliyofanyika Jumalililopita.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumapili ya November 4 mwaka 2018 ilifanikiwa kupata viongozi wake wakuu sambamba na uchaguzi mkuu wa mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Simba SC ambapo kura zilihesabiwa hadi alfajiri ya November 5 2018.

Baada ya uchaguzi kufanyika Swed Mkwabi ambaye alikuwa ndio mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti amepita bila kupingwa kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote  (kura 1579), hata hivyo washindi wa nafsi za ujumbe wamepatikana watano ambao ni Asha Baraka, Hussein Kitta, Dr Zawadi Kadunda, Mwina Kaduguda na Selemani Said.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents