Burudani ya Michezo Live

Picha: Uchukuaji video ya wimbo mpya wa MwanaFA ft. Kilimanjaro Band & Mandojo na Domokaya

IMG_3681 (640x427)

Uchukuaji picha wa video ya wimbo mpya wa rapper Hamis Mwinjuma aka MwanaFA aliyoishirikisha bendi kongwe ya Kilimanjaro Band aka wananjenje na Mandojo na Domokaya umeanza rasmi leo jijini Dar es Salaam chini ya director Karabani.

“Karabani anaishoot hii video lakini inapelekwa South Africa kama ilivyoripotiwa na watu wa God Father ndio wanaedit hii video na sababu yangu ilikuwa ni kwamba ningekuwa nimefanya peke yangu ningeenda kuifanya South Africa lakini una band, una watu sita, saba una Mandojo na Domo Kaya watu tisa na mimi ni wa kumi, wimbo mmoja ungenitia umaskini hapo hapo, yaani naweza kufanya lakini ningeumwa mpaka mwezi wa sita,” amesema MwanaFA. “Kwa gharama zilivyo tukaona hakuna sababu jamaa wanasema mara nyingi hata sisi tunapata picha nzuri tatizo linakuja kwenye editing. Vitu hivi pia vina politics, watu wanatumia connections walizonazo, Godfather akifanya una uhakika wa kwenda Trace, una uhakika wa kwenda MTV Base una uhakika wa kwenda Channel O kama kawa yaani.”

Akizungumzia sababu za kuichagua band ya Kilimanjaro FA amesema, “ Unajua suala ni kwamba unatafuta angle tofauti, sijakaa kwenye muziki kwa miaka 12 for no good reason yaani kulikuwa na sababu ya mimi kubaki na kwasababu natafuta angle mpya kila siku ya kutokea. Sijawahi kujisikia vizuri kuperform nyimbo yangu kama nilivyojisikia wakati naperform na Njenje kwahiyo nikaona hawa ndio band ambayo nataka kuitumia Plus Njenje ina miaka 42 inafanya muziki kwahiyo kama unataka kutengeneza picha ya ulegendary lazima kila kitu kiwe na picha hiyo, siwezi kuchukua bendi za watoto wadogo wakati bendi ya malegendary ipo.”

Aidha MwanaFA amesema anashow inakuja hivi karibuni aliyoipa jina la The Finest na atakayoshirikiana na bendi hiyo pamoja na wasanii aliowahi kuwashirikisha kwenye nyimbo zake. “The Finest iliripotiwa kama wimbo lakini The Finest actually ni show sio wimbo. Ni show ya mara moja, hatutaki kuifanya sana itakuwa ni kitu kinachozoeleka, sio ya watu wengi ni show wanayohudhuria watu kama 500, corporate show. Tunachojaribu ni kuuvusha muziki, unajua aina ya muziki tunaoufanya mara nyingi unaonekana ni muziki wa watu fulani.

Kilichobaki ni kwamba huu muziki unahitaji hela na unahitaji hela kutoka kwenye corporations na sio hata mauzo ya muziki. Corporations zinatakiwa ziweke hela kwenye muziki na namna ambayo tunatakiwa kuzishawishi kufanya hivyo ni kwa kuwaonesha kwamba muziki wetu una nguvu kiasi gani, muziki wetu ni mzuri kiasi gani na ndio hiyo idea ya The Finest ilipokuja.”

Hizi ni baadhi ya picha za uchukuaji wa video hiyo.

IMG_3658 (640x427)

Karabani
Karabani

IMG_3660 (640x427)

Msaidizi wa Karabani
Msaidizi wa Karabani
Karabani akiwa kazini
Karabani akiwa kazini

IMG_3667 (640x427)

IMG_3669 (640x427)

IMG_3671 (640x427)

IMG_3672 (640x427)

IMG_3677 (640x427)

MwanaFA, Bill na Domokaya
MwanaFA, Bill na Domokaya
MwanaFa, Bill the African na Mandojo
MwanaFa, Bill the African na Mandojo
Mandojo
Mandojo

IMG_3681 (640x427)

Domokaya
Domokaya

IMG_3686 (640x427)

IMG_3691 (640x427)

IMG_3693 (640x427)

IMG_3695 (640x427)

IMG_3698 (640x427)

Lucy - Model True Eyes Modeling Agency
Lucy – Model True Eyes Modeling Agency

IMG_3712 (640x427)

Magdalena
Magdalena
Eunice
Eunice
MwaJ
MwaJ

IMG_3727 (640x427)

Magdalena na MwaJ wa True Eyes Modeling Agency watakaotumika kwenye video hiyo
Magdalena na MwaJ wa True Eyes Modeling Agency watakaotumika kwenye video hiyo

IMG_3729 (640x427)

IMG_3730 (640x427)

IMG_3750 (640x427)

IMG_3754 (640x427)

IMG_3756 (640x427)

Mpiga saxophone wa Kilimanjaro Band
Mpiga saxophone wa Kilimanjaro Band

IMG_3768 (640x427)

IMG_3770 (640x427)

IMG_3772 (640x427)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW