Picha: Wasanii waungana na Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Slaa kwenye kampeni ya uchangishaji madawati
Wasanii wa sanaa za uchoraji nchini, wameungana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa kwenye kampeni yake ya kila mwaka (Mayor’s Ball) kuchangisha madawati kwaajili ya shule za manispaa hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni mchoraji Robino Ntila
Ili kusaidia uchangishaji wa fedha hizo Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel itaendesha mnada wa hisani ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kununua madawati. Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, mstahiki meya huyo aliishukuru Hyatt Regency kwa msaada wake wa kudhamini shughuli hiyo ambapo jumla ya wasanii 10 watakaa kwenye hoteli hiyo kwa siku tano na kuchora picha mbalimbali zitakazopigwa mnada kwaajili ya kampeni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel, Trevor Saldanha
Trevor Saldanha akiongea na waandishi wa habari
Picha hizo zitauzwa kwa wageni waalikwa watakaohudhuria mnada huo wa hisani utakaofanyika November 16.
Mstahiki Meya Slaa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari leo
Akiongea kwenye mkutano huo kiongozi wa jopo hilo la wachoraji, Robert Ntilo, alisema, “Huu ni mradi wawa kipekee wa Meya Silaa na tunajivunia kualikwa kushiriki na kutumia vipaji vyetu, tunaweza kuleta tofauti.”
Robert Ntilo
Wasanii watakaoshiriki kuchora ni pamoja na Robino Ntila, Aggrey Mwasha, Salum Kambi, Cuthbert Semgoja, James Haule, Haji Chilonga,Thobias Minzi, Moses Luhanga, Poni Yengi Miss na Vita Malulu.
Miongoni mwa wachoraji 10 watakaochora picha zitakazopigwa mnada November 16
Kampeni ya mwaka huu imepewa jina la ‘Dawati ni Elimu’ ikiwa na msemo ‘Kalisha mmoja, boresha Elimu’.
Dhruv Jog wa Advent Construction Ltd
Katika kampeni mwaka huu matembezi ya hisani yalifanyika October 12 kuanzia Mnazi Mmoja hadi shule ya msingi ya Bunge na yaliongozwa na Mama Salma Kikwete ili kukuza uelewa juu ya kampeni hiyo yenye lengo la kukusanya shilingi bilioni 4.98.
Fedha hizo zitatumika kununua madawati 30,487 kwaajili ya shule za manispaa ya Ilala.
.