Burudani ya Michezo Live

Pochettino kurithi mikoba ya Solskjaer Man United, kumng’oa Rafael Benitez ndani ya Newcastle inahitaji ubavu

Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumrithi Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Manchester United. (Manchester Evening News)

Image result for Man Utd stance on sacking Ole Gunnar Solskjaer as Mauricio Pochettino keen to replace boss

Tottenham wapo tayari kupokea ofa za usajili za chini ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)

Spurs haina mpango wa kumsajili kiungo Mserbia anayechezea Manchester United Nemanja Matic, 31. (Manchester Evening News)

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni “uozo” japo “haiwezekani kurudi nyuma”. (Mirror)

Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal – in Spanish)Kocha wa Tottenham Jose Mourinho

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)

Kocha wa Manchester United Solskjaer amesema anataka klabu hiyo kufanya maamuzi ya haraka katika dirisha la usajili, akiashiria kuwa mwenyekiti mtendaji Ed Woodward hakufanya maamuzi ya haraka mwishoni mwa msimu wa uliopita. (Evening Standard)

Manchester City wameingia katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez. Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Sky Sports Italia, via Calciomercato – in Italian)

Mshambuliaji raia wa Ufaransa Olivier Giroud atafanya mazungumzo magumu na klabu yake ya Chelsea. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 anataka kuondoka klabuni hapo mwezi Januari. (Evening Standard)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefanya maamuzi ya kutofanya usajili wowote mwezi Januari licha ya klabu hiyo kupwaya kwenye safu ya ulinzi. (Independent)

Klabu yeyote ya ligi kuu Uingereza ambayo itataka kumsajili kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez italazimika kulipa fidia ya zaidi ya pauni milioni 20 kwa klabu yake ya sasa, Dalian Yifang ya Uchina. (Mail)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW