Habari

Polisi watumia vilipuzi vyakutoa machozi kuutawanya mkutano wa William Ruto

Polisi nchini Kenya wamelazimika kutumia vilipuzi vya kutoa machozi ili kuutawanya umati mkubwa uliokusanyika kwa ajili ya mchango, uliotarajiwa kuhudhuriwa na makamu wa raisi wa Kenya William Rito. Mkutano huo ambao ulikua umepangiwa kufanyika mjini Nyamira, ambapo wabunge wa kaunti hii walikua wamepanga kujumuika na Ruto katika kuchangisha pesa.

Hata hivyo habari za ndani, zinasema kua makamu wa raisi William Ruto ameapa kuendele na ratiba hiyo ya kuchangisha jumatatu ijayo. Ruto amekua akionekana akipiga kampeni za mapema kuwania kiti cha uraisi mwaka 2022, hali ambayo inapingwa vikali na raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta na wadau wwngine wakuu serekalini.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai – Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents