Habari

Nigeria: Mtu mmoja ahukumiwa kifo baada ya kukiri kuwanyonga wanawake tisa

Mwanaume aliyewaua wanawake tisa na kesi yake ikaibua ghadhabu amehukumiwa kunyongwa katika mjini wa kusini wa Port Harcourt.

Waendesha mashtaka wamesema mwanaume huyo, mwenye miaka 26, Gracious David-West aliwanyonga wanawake hao katika hoteli mbalimbali nchini Nigeria alikokuwa anakutana nao kati ya mwezi Julai na Septemba 2019

Jaji Adolphus Enebeli amesema kifo chake kitatekelezwa kwa kunyongwa. Hukumu hiyo ya kifo ni nadra sana kutolewa nchini Nigeria — hukumu ya kifo mara ya mwisho kutolewa ilikuwa ni mwaka 2016 kwa watu watatu.

Mmoja wa waathirika alinusurika na shambulio lake lakini hakuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi wakati kesi hiyo inaendelea.

Serikali imesema kwamba mwathirika huyo hajulikani alipo licha ya kuombwa asitoroke.

Polisi imesema mshtakiwa pia naye alikiri kutekeleza mauaji ya wanawake wengine sita. Mamlaka inasema mauaji hayo yalitokea baada ya mtuhumiwa kufanya ngono nao na baada ya hapo aliwanyonga kwa kutumia shuka jeupe.Waathirika walikuwa wanafanya kazi ya kujiuza miili yao.Mwanzoni mwa kesi hiyo mtuhumiwa alikiri kuwa na hatia lakini jaji alitaka kesi hiyo kuendelea kusikilizwa kutokana na uzito wa uhalifu.

Kwa muda, mamlaka iliisitisha na kutafuta ushaidi ambao ulisikilizwa mahakamani.

Polisi wanasema David West alikuwa akiwaua wanawake mwenyewe bila ushirika na mtu

Wakati wa mfululizo wa mauaji ya wanawake hao mwezi Septemba mwaka jana, raia wenye hasira waliandamana barabarani na kuitaka mamlaka kuchukua hatua kutatua tatizo hilo. Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 19, wakati akijaribu kuondoka Port Harcourt wakati ambapo mamlaka ilikuwa karibu kumkuta na hatia.

Picha za video za CCTV zilimpiga picha akiwa anaondoka hotelini na picha hizo zilienea katika mitandao ya kijamii.

Watu wa usalama walimkuta katika basi akisafiri kutoka Uyo katika jimbo la Akwa Ibom , ambako ni mbali kutoka Port Harcourt kwa dakika 45.

Tunafahamu nini kuhusu muuaji?

David-Westa alizaliwa katika mji wa wavuvi wa jimbo la Buguma, eneo ambalo linafahamika sana kwa kutengeneza mafuta na fukwe zake kuwa za kuvutia.

Polisi wanasema David-West alikuwa mjumbe wa kikundi cha wanamgambo wa kigaidi kijulikanacho kama Greenlanders – au Dey Gbam.Wale waliomfahamu waliiambia BBC kuwa alikuwa mtoto wa pekee katika familia , ingawa mama yake na baba yake walikuwa wanaishi tofauti.

Waandishi waliomuona mahakamani walimuelezea tabia yake kuwa haieleweki.

“Alikuwa na hasira sana, alikuwa anamkatisha jaji kila mara na alikuwa anataka kujitetea mwenyewe licha ya kuwa na wakili,” alisema mwandishi Alwell Ene.

Alitimia hoteli za bei nafuu ambazo hazina usalama mzuri kama kuwa na kamera za CCTV, katikati ya mji wa Port Harcourt, kwa mujibu wa polisi.

Waliouawa ni kina nani?

Hawakufahamika sana waathirika ni kina nani ila majina yao yalitajwa.

  • Maureen Ewuru
  • Jennifer Nwokocha
  • Linda Waripa
  • Dorcas Francis
  • Blessing Effiong
  • Rose Samuel
  • Kelechi Bridget Onuoha
  • Patience Hamo
  • Antonia Ibe

Mwandishi wa BBC, Karina Igonikon huko Port Harcourt amesema marafiki na ndugu wa marehemu hawakuonekana mahakamani, isipokuwa siku ya kwanza ya kusikilizwa kwa hukumu hiyo baba wa mmoja wa wahanga alihudhuria.

“Ni kama wahanga hawakuwa na wapendwa wao, hakuna anuani wala chochote kuhusiana na hao,”alisema.

Polisi walisema pia mtuhumiwa alikiri kuuwa wanawake wengine sita katika mji wa Abia, Imo, Edo, Lagos na jimbo la Edo lakini hakuchukuliwa hatua kwa mauaji hayo.

Ramani

“Hakuna aliyekuja kuongelea vifo ambavyo vilikuwa na ushaidi mdogo ili kumbana aeleze ukweli,” mwendesha mashtaka Chidi Ekeh aliiambia BBC.

Kulikuwa na mvutano kuhusu utambulisho wa wanawake hao na jinsi walivyomfuata muuaji mpaka hotelini.

Wachunguzi wanasema alikuwa anawadanganya waathirika kwa kudai kuwa ni afisa wa jeshi na kuahidi kuwalipa kiwango kikubwa cha fedha. Mwathirika mmoja , Jennifer Nwokocha, alidaiwa kuwa alifika Port Harcourt kutoka Lagos kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Meneja wa hoteli aliyeutupa mwili wa mmoja wa waliouawa mbele ya jengo hili la makazi pia ameshtakiwa

“Walikutana hotelini ambako alikuwa anakaa na kupata vinywaji ,walibadilishana namba na kukutana baadae usiku,” mchunguzi aliiambia BBC.Polisi wanasema alikuwa anawatishia wanawake kwa kisu na kuwazuia wasipige kelele.

Kabla ya kuwaua aliwaibia fedha , kadi ya kutolea fedha benki na vitu vingine vya thamani.

“Tulikuta waathirika wakiwa hawana nguo, shingo zao zikiwa zimezungushiwa nguo na pia walizungushiwa vitambaa mikononi na miguuni.

“Ingawa hakuna ushahidi haswa unaoainisha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kishirikina ila yanahusishwa kuwa ya aina hiyo,” Bwana Ekeh aliiambia BBC.

Wale waliopona

Benita Etim, mwenye miaka 23-anafanya kazi ya kujiuza mwili ,alinusurika kuuwawa na muuaji huyo.Hakutoa ushahidi mahakamani ingawa aliambiwa na mamlaka asitoke nje mji.

Katika mahojiano na BBC mwezi Septemba mwaka jana alisimulia jinsi alivyokutana na mwanaume huyo Agosti 18 na alimfungia katika chumba cha hotelini.Alielezea jinsi alivyobakwa na kutishiwa kisu na kufungwa kwenye kiti.

“Alikata kipande cha shuka na kufunga mikono yangu na miguu katika kiti na kutumia kitambaa kingine kufunga mdomo wangu.

“nilipiga kelele lakini hakuna aliyenisikia kwasababu alikuwa ameweka sauti kubwa ya TV na jenereta ilikuwa inaunguruma karibu na chumba hicho,”alisema.

“Nilimuomba asiniue.”

Aliondoka kwenye chumba hicho akiwa na simu yangu na hakurejea.

Wafanyakazi wa hoteli walimkuta siku iliyofuata akiwa bado anapiga kelele kuomba msaada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents