Michezo

Poulsen ageuza Kambi ya Stars Jeshi

 

Tofauti na kanuni zilizowekwa na utaratibu wa kocha mkuu wa Stars Jan Poulsen kwenye kambi inayojiandaa kwa mechi dhidi ya Morocco, zimewakosesha wachezaji uhuru wa kufanya baadhi ya mambo yao kutokana na kuwa chini ya uwangalizi makini kama vile wako jeshini.

Stars imeweka kambi hiyo Hotel ya The Atriums iliyopo sinza ikijiandaa kuivaa Morocco octoba 9 kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni harakati za kufuzu katika kombe la mataifa ya Afrika (can 2012)itakayo fanyika Gabon na Equatorial Guinea.

Kwa mujibu wa chanzo habari ya kutoka ndani ya kambi hiyo kimeiambia bongo5 kuwa utaratibu unatofauti mkubwa tangu Poulsen akabidhiwe jukumu hilo, ikiwemo kukaa na wachezaji Hoteli moja tofauti na aliyekuwa kocha aliyepita Mbrazili Marcio Maximo.

Kanuni na taratibu zetu mpya zilizopo kwenye kambi yetu nin gumu tofauti na Maximo, Poulsen muda wote kuwepo kambini na anakaa getini akisoma kitabu miguu juu ya stuli hali hali inayotunyima uhuru wa kutoka.’ Alisema mchezaji mmoja kutoka stars.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents