Habari

Programu ya Funguka kwa Waziri yatatua migogoro ya Ardhi 628 kwa siku tano Dar

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepongezwa na wananchi wa Dar es Salaam kwa uamuzi wake wa kukutana nao na kutatua migogoro ya ardhi 628 katika Mkoa huo.


Imeelezwa kuwa amefanikisha kazi hiyo katika kipindi cha siku tano kupitia programu ya Funguka kwa Waziri akifanya kazi hadi saa nne usiku.

Lukuvi alihitimisha programu ya Funguka kwa Waziri kwa kukutana na wananchi wa Manispaa ya Kinondoni hapo jana tarehe 22 Februari kwa kusikiliza na kutatua kero, malalamiko na migogoro 300 iliyomfikisha saa 4:22 usiku.

Awali, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alikutana na wananchi wa Manispaa za Ilala ambapo alishughulikia migogoro 122, Ubungo 75, Kigamboni migogoro 65 na Manispaa ya Temeke migogoro 66 na kufanya jumla ya migogoro aliyoishughulikia kwa siku zote tano kufikia 628.

Kwa mujibu wa Azam Tv, Kati ya wananchi aliokutana nao tangu kuanza kwa program hiyo siku ya Jumanne tarehe 18 Februari 2020, Manispaa ya Kinondoni ilioonekana kuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye malalamiko ya ardhi ukilinganisha na Manispaa nyingine za mkoa wa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents