Michezo

Promota Eddie Hearn amuonya bondia Anthony Joshua

Eddie Hearn ambaye ni promote maarufu wa mapambano ya ngumi amemuonya bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Anthony Joshua kuweka fikra zake zaidi katika kuulinda ubingwa wake huo katika siku za usoni.

Promota wa maarufu wa ngumi, Eddie Hearn

Hearn amesema hayo kutokana na kuanza kumuona bondia huyo wa Uingereza kaanza kuridhika na mafanikio aliyoanza kuyapata.

Bondia Anthony Joshua (kulia) akimuangusha mpinzani wake Wladimir Klitschko(kushoto) na kuelekea chini

Promota huyo aesisitiza kuwa Joshua ni lazima ajiandae kikamilifu kwa kuwa anakabiliwa na mapambano makubwa mbele yake na hivyo asisubiri mpaka bodi imjadili.

Joshua anashikilia ubingwa wa uzito wa juu IBF pamoja na WBA   ambapo bodi ya mchezo wa ngumi inamuhitaji bondia huyo kuitetea mikanda hiyo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents