Michezo

Rafinha awa kikwazo usajili wa Pogba Kutua Nou Camp

Rafinha awa kikwazo usajili wa Pogba Kutua Nou Camp

Katika miongoni mwa tetesi za usajili zinazosumbua katika mitandao ya kijamii ni ule unaomuhusu kiungo Mfaransa anayekipiga katika klabu ya Manchester United Paul Labille Pogba ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia katika klabu ya FC Barcelona.

Soccer Football – Premier League – Manchester United v Leicester City – Old Trafford, Manchester, Britain – August 10, 2018 Manchester United’s Paul Pogba Action Images via Reuters/Andrew Boyers EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/le

Viongozi wa Barcelona walisema kuwa bado wanahitaji kufanya usajili mwingine mkubwa na moja kwa moja habari hizo zilipokelewa kuwa inawezekana akawa Pogba,na watu wengi wajahusisha kitendo cha kiungo huyo kuonekana hana furaha katika mchezo wa wa ufunguzi dhidi ya Leicester City na baada ya kuhojiwa Pogba alidai kuna kitu kinamfanya awe hivyo ila kikaa sawa ndo atakuwa na furaha.

Mapema leo Mkurugenzi wa Barcelona Ariedo Braida amesema klabu hiyo haiwezi tena  kujaribu kumsaini Paul Pogba wa Manchester United mwezi huu kwani kiungo wao Rafinha ameamua kubaki kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake  Camp Nou.

Mkurugenzi huyo aliiambia Radio Sportiva kuwa “Sidhani kama tutaendelea kumfuatilia Pogba, Ingawa mchezaji mzuri tena wa kimataifa,”

 


“Rafinha, labda,kama ataamua kuondoka Barcelona,” Braida alisema. “Yeye ni mtu mwenye ubora mzuri, pia ni mchezaji anayeweza kuamua mchezo kwa njia ya kushughulikia mpira ipasavyo – anaweza kufanya makubwa zaidi”.

“Mwaka jana, alirudi nyumbani kutokana na majeraha mabaya, lakini alipopona alifanya vitu vingi kwa Inter. Yeye ni mchezaji ambaye ana ujuzi wa kiufundi zaidi na anaifaa Barca vizuri.”

FC Barcelona wamekuwa na hitajio la kiungo mzuri kutokana na kuondoka kwa Iniesta pamoja na Bosquet kuonekana umri wake hauruhusu kupambna zaidi uwanjani anahitaji mpira wa taratibu.

 

By Ally Juma

 

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents