Michezo

Raheem Sterling aeleza sababu ya kujitoa katika timu ya taifa ya England

Raheem Sterling aeleza sababu ya kujitoa katika timu ya taifa ya England

Mchezaji wa klabu ya Manchester City  na timu ya taifa ya England Raheem Sterling amejitoa katika kikosi cha England chini ya kocha wake Southgate katika mechi dhidi ya Uhispania na Uswizi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameamua kujitoa kwenye kikosi hicho kwa sababu anaumwa mgongo,shirikisho la soka nchini England limesema Sterling ndiye mchezaji pekee atakayekosekana wakati timu hiyo ilikapoteremka dimbani St George Jumatatu.

hadi sasa hakuna mchezaji aliyepangwa kuichukua nafasi yake, hatua inayomuacha meneja Gareth Southgate akiwana kikosi cha wachezaji 22 atakaowatumia katika mchuano ya Ulaya ya ligi ya kitaifa ya UEFA pia dhidi ya Uhispania na Jumanne katika mchuano wa kirafiki na Uswizi.

katika kikosi hicho cha Southgate hawa ndio wachezaji atakaowatumia:-

Makipa: Jack Butland (Stoke), Jordan Pickford (Everton), Alex McCarthy (Southampton)

Walinzi: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Fabian Delph (Manchester City), Joe Gomez (Liverpool), Harry Maguire (Leicester City) Danny Rose (Tottenham Hotspur), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City), James Tarkowski (Burnley), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Kyle Walker (Manchester City)

Wachezaji kiungo cha kati: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Manchester United), Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)

Wachezaji kiungo cha mbele: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Danny Welbeck (Arsenal)

 

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents