Michezo

Raheem Sterling ashindwa kuingia kandarasi mpya na Man City

Kiungo wa klabu ya Manchester City, Raheem Sterling ameshindwa kufikia makubaliano ya kuongeza kandarasi kuendelea kuitumikia timu hiyo utakao mfikisha hadi mwaka 2022.

Baadhi ya vyanzo vya habari vinaeleza kuwa pande zote mbili zimeshindwa kufikia muafaka hasa katika eneo la maslahi ya mshahara na kushidwa kupanga ni lini watakutana kujadili upya swala hilo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amejiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza na kuelekea nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la Dunia hii leo siku ya Jumanne.

Sterling amefunga jumla ya mabao 23 kwenye michezo yote ya ligi kuu nchini Uingereza huku ikiaminika kuwa mazungumzo yake na City yatakamilika kabla ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia.

Inapata miezi sasa City imekuwa na mpango wa kufanya mazungumzo na wachezaji wake muhimu akiwemo, Kevin De Bruyne, Fernandinho, David Silva na Nicolas Otamendi.

De Bruyne akiwa amekubali kandarasi mpya ya miaka sita mwezi Januari ambapo atakuwa akipokea kitita cha paun 350,000 kwa wiki. Sterling amewasli hapo akitokea Liverpool kwa dau lililoweka rekodi ya pauni milioni 44 mwaka 2015 na kufanikiwa kumaliza nyuma ya kinara wa mabao, Sergio Aguero katika upachikaji magoli.

Hatma ya Sterling itajulikana mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents