Michezo

Rais Donald Trump atofautiana na wanamichezo

Kumekuwa na wamarekani weusi ambao wanapinga sera za Rais mpya, Donald Trump hali ambayo imefikia mpaka wana michezo mbalimbali kuingia katika sakata hilo na kuonyesha hisia zao.

Wachezaji wa timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars za marekani  nimiongoni mwa wanamichezo ambao wameonyesha kutofurahia na sera za Trump  baada ya kushindwa kuheshimu wimbo wa taifa wa marekani ulipokuwa ukipigwa katika uwanja wa Wimbley ikiwa ni inshara ya kuonyesha umoja wa kumpinga Rais huyo.

Mmmiliki wa timu ya Jaguars, Shahid Khan ambaye alitoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 740,000 katika kumuunga mkono Trump wakati wa kampeni  aliungana na wachezaji wake katika kupinga yanayo fanywa na Rais huyo.

Kupitia mtandao wa kijamii siku ya Ijumaa, Rais wa Marekani, Trump ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kulaani walichokifanya wachezaji kukaidi kuheshimu wimbo wa taifa.

Mfalme wa mchezo wa basketbaal, Steph Curry yeye alianika hisia zake wazi kwakusema kuwa kamwe hatokanyaga Ikulu ya Marekani, White House ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hisia zake za kupinga sera hizo huku akiamini kuwa kwa kufanya kitendo hicho kitakuwa mbolea ambayo italeta mafanikio kwa wengine kufuata nyayo zake kwakuwa anataka kuionyesha dunia hisia zake juu ya utendaji kazi wa raisi huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents