Aisee DSTV!

Rais Kenyatta azunguzmia kipigo cha Taifa Stars dhidi ya Kenya “Juzi tumechapana Cairo, nafikiri hakuna aliyelala siku hiyo”(+Video)

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya yupo nchini kwaajili ya ziara ya siku mbili akiwa na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli Mkoani Chato. Akiwa huko Rais Kenyatta hakusita kugusia matokeo ya mchezo wa Mataifa ya Afrika Afcon, baina ya Tanzania dhidi ya Kenya ambayo Taifa Stars ikikubali kipigo cha mabao 3 – 2 dhidi ya majirani zao Kenya.

Akizungumza katika hadhara, Rais Kenyatta amesema siku hiyo zilipokutana timuhiyo hakuna mtu alielala na hiyo ndiyo hali ya kimchezo na Kenya kufanikiwa kuipiga Taifa Stars.

“Juzi tumechapana kule Cairo, Misri. Kila mtu na timu yake, Harambee Stars na Taifa Stars nafikiri siku hiyo hakuna mtu aliyelala. Lakini hiyo ndiyo hali michezo, tulishindana safari hii Kenya ikaipiga Taifa Stars.”- Amesema Rais Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameongeza “Lakini nyinyi mlifaidika tulipocheza na Senagl tulichwa mbili na nyinyi mkapigwa tatu. Hivyo tujikakamuwe tusiwe tunatolewa katika mzunguko wa kwanza.”

“Tuwe tunafika fainali na hapo tukutane Kenya na Tanzania, ndiyo Tanzania ikishinda Kenya imeshinda, kwa sababu marafiki mambo yao ndivyo yanavyokwenda.”

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema

“Uhuru Kenyatta amekuja kuniomba msamaha kwa sababu ametufunga mabao 3 – 2 , kwa sababu tulikubaliana tufungane magoli 2 – 2. Tulipofunga lapili sisi tukatulia yeye akaongeza latatu, kwahiyo nikasema ngoja ni msubiri atakuja kuomba msamaha.”- Amesema Rais Magufuli

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW