Habari

Rais Magufuli afanya uteuzi wa RC, KM, NKM na DC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Julai 2020 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo.

BREAKING: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA USIKU HUU - YouTube

Kwanza, Mhe Rais Magufuli amemteua Dkt Jummanne Fhika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya uteuzi huo Dkt Fhika alikuwa Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Bw.Christopher Ole Sendeka

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Nzuki alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Malihasili na Utalii na anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda.

Tatu Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Sanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Prof. Kitila Alexander Mkumbo.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Dkt. Allan Kijazi anachukua nafasi ya Dkt. Aloyce Nzuki aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na pia Dkt. Allan Kijazi ataendelea kuwa Kamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents