Rais Museveni atoa kibonzo cha video yake akicheza wimbo wa Jerusalema (+ Video)

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa video ya kibonzo chake akicheza densi ya wimbo uliovuma wa Jerusalema.

Densi ya Jerusalema ilikuwa ni densi iliyovuma na kuchezwa kote duniani mwaka jana, kupitia kampeni ya mtandao iliyojulikana kama #Jerusalemachallenge baada ya kutolewa kwa wimbo wa Jerusalema na mwanamuziki wa Afrika Kusini Master KG.

Rais Museveni amesema kuwa ametoa video hiyo baada ya kushawishiwa na wafuasi wake vijana.

Waganda watapiga kura Alhamisi wiki hii kuwachagua wabunge na rais.

Bw Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35, anawania muhula wa sita. Jumla ya wagombea 11 wanawania kiti cha urais akiwemo mwanamke mmoja.

Bofya hapa chini kuitazama.

https://www.instagram.com/tv/CJ8H5JoB3ud/

https://www.instagram.com/tv/CJ8H5JoB3ud/

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW