Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Rais wa La Liga, Tebas asisitiza Ronaldo na Griezmann wataendelea kusalia Hispania

Rais wa ligi kuu nchini Hipsania (La Liga), Javier Tebas anaamini kuwa mshambuliaji bora wa dunia wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo na mchezaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann watasalia msimu huu.

Kupitia Radio Onda Cero ya nchini Hispania rais huyo wa LaLiga, Tebas anaamini kuwa wachezaji hao wataongeza mikataba kwenye timu zao msimu huu wa usajili huku akiamini kuwa hakuna athari zozote zitakazo jitokeza endapo Ronaldo ataamua kutimkia kwenye ligi nyingine.

”Nafikiri kwamba Cristiano ataendelea kusalia ndani ya klabu ya Real Madrid na Antoine Griezmann atakuwepo Atletico. Kama Cristiano Ronaldo ataondoka hakutokuwa na tatizo ndani ya LaLiga,” amesema Tebas.

Ronaldo alitangaza kucheza mchezo wake wa mwisho wa ligi hiyo mwezi uliyopita akiwa Real Madrid wakati nyota wa Atletico Madrid, Griezmann akihitajika na Barcelona.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW