Michezo

Rais wa Madrid, Florentino Perez ampigia magoti Ronaldo

Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amesema bado haja wasiliana na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo kuzungumzia juu ya mustakabali wa maisha yake ya baadae ya soka.

Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez(kushoto) akiwa na Cristiano Ronaldo(kulia)

Perez amesema anatarajia kufanya maongezi na mchezaji huyo haraka iwezekanavyo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya mabara ambayo inaendelea nchini Urusi.

Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez(kulia) akiwa na Cristiano Ronaldo(kushoto)

“Kwa vyovyote vile lazima kunakitu kitakuwa kimetokea, kitu ambacho kitakuwa kimemgusa na kumuathiri, ni muaminifu sana nina uhakika atatuambia na tutaangalia cha kufanya. Kwa bahati mbaya yeye kwa sasa yupo katika mashindano muhimu ya Mabara, hasa katika kufikia mafanikio yake katika mchezo wa Mpira pamoja na timu ya Taifa ya Ureno hivyo sahitaji kuwasumbua,” amesema Perez.

“Hizi ni habari za ghafla, nitapambana kwa gharama zozote kama mchezaji na kama mtu tu wakawaida kulimaliza jambo hili. Cristiano ni kijana mzuri na mwenye kipaji ni nachoweza sema kilamtu ni lazima atimize wajibu wake wa kulipa kodi na sina shaka naye ataweza kupambana nalo na kulimaliza,” ameongeza.

Perez amekiambia kituo cha Radio cha Onda Cero cha nchini Hispania

Siku chache zilizopita Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, alisema anahitaji kuondoka Hispania kufuatia kuingia katika shutuma za ukwepaji kodi takriban kiasi cha paundi milioni 13.

Ronaldo alisaini mkataba wa miaka 5 mwezi Novemba mwaka 2016 kuendelea kukitumikia kikosi hicho cha Madrid na kwa sasa anahitaji kurejea Manchester United.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents