Michezo
Ratiba nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya yatoka
Ratiba ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya imepangwa huko Nyon, Uswiss.
Ratiba inaonyesha FC Barcelona itakipiga dhidi ya FC Bayern Munich. Guardiola na Luis Enrique walikuwa kwenye kikosi kimoja cha Barca kilichokuwa kikifundishwa na Van Gaal msimu wa 1999/2000.
Kwa upande mwingine mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid watacheza dhidi ya Juventus. Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Mei 5 na 6 na marudiano zitakuwa wiki moja itakayofuatia ya tarehe 12 na 13.