Michezo

Ratiba ya ligi kuu Bara yatoka, Simba na Yanga kukutana mwezi huu Dar

Ratiba ya ligi kuu Bara yatoka, Simba na Yanga kukutana mwezi huu Dar

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura limetangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 itakayoanza Agosti 22 2018.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Wambura amesema kuwa ligi hiyo itahusisha jumla ya mechi 380 kutoka 240 ambazo zilichezwa msimu uliyopita kutokana na ongezeko la timu.

Wambura ameeleza kuwa msimu wa mwaka 2017/18 ligi ilihusisha jumla ya timu 16 pekee lakini kuelekea msimu ujao kutakuwa na jumla ya timu 20 ambazo zimefanya kuwe na ongezeko hilo la idadi za mechi.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo mechi zitakazoanza Agosti 22 ni baina ya Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting vs  Ndanda FC, Singida United United dhidi ya Biashara FC, Alliance FC dhidi ya Mbao FC pamoja na Kagera Sugar watakaocheza na Mwadui FC.

Huku mechi yenye msisimko mkubwa nchini ya watani wa jadi, Simba na Yanga ikitarajiwa kuchezwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents