MichezoUncategorized

Rekodi hii mbovu ya Olivier Giroud nchini Urusi yamuangusha kocha wa Ufaransa

Meneja wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kuwa hawezi kumuacha straika wake, Olivier Giroud kwenye mchezo wao wa nusu fainali licha ya nyota huyo wa Chelsea kushindwa kufunga goli hata moja kwenye michuano ya kombe la dunia inayo endelea nchini Urusi.

Giroud mwenye umri wa miaka 31, ameanza kwenye michezo yote minne ambayo Ufaransa imecheza lakini ameshindwa kabisa kufunga hata bao moja ikiwemo mechi yao ya Ijumaa hii waliyo ibuka na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Uruguay.

Meneja huyo wa Les Bleus, Deschamps amesema ni kweli Olivier hajafumania nyavu bado lakini wacha nirejee kusema tena muda wake bado.

Ni kweli mnayosema kuwa Olivier hajafunga goli mpaka sasa, naruria tena kusema muda wake bado. Pengine hajakuwa sawa na aina ya uchezaji ambao wenzake wanacheza lakini timu inamuhitaji kwa kilakitu hii ni kwa sababu licha ya kuwa hajafunga lakini amefanya mambo mengi kwetu.

Wakati wa zama zake, Deschamps akiwa mchezaji wa Ufaransa nafasi ya kiungo walipo twaa ubingwa huo mwaka 1998 ,  ndani ya kikosi hicho alikuwepo straika, Stephane Guivarc’h ambaye alicheza jumla dakika 268 kwenye mashindano hayo pasipo kufunga goli hata moja.

Giroud amerithi mikoba ya Guivarc’h
Mchezaji Dakika alizopata kucheza Mashuti aliyopiga Mashuti yaliyolenga lango Mabao
Stephane Guivarc’h 1998 268 16 3 0
Olivier Giroud 2018 380 7 0 0

 

Wakati, Giroud akitumia dakika zote hizo pasipo hata kufumania nyavu mwenake Harry Kane ambaye ni mchezaji wa Uingereza anawania kiatu cha dhahabu kwenye michuano hiyo baada ya kufunga mabao sita akicheza michezo mitatu akitumia dakika 273 baada ya kupiga mashuti tisa pekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents