Michezo

Robin van Persie kutocheza kwa wiki 4 – 6 kutokana na kuumia goti

Mshambuliaji wa Manchester United,Robin Van Persie atakuwa njeeya uwanja kwa wiki 4-6 baada ya kufanyiwa vipimo kiundani nakugundulika amepata majereha kwenye goti katika mchezo wa kufuzu robo fainali ya UEFA Jumatano wiki hii.

Robin van Persie  akitolewa njee ya uwanja baada ya kuumia katika mchezo wa kufuzu robo fainali
Robin van Persie akitolewa njee ya uwanja baada ya kuumia katika mchezo wa kufuzu robo fainali ya UEFA.

Van Persie ambaye alifunga mabao matatu yaliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali ya UEFA dhidi ya Olympiacos, aliumia goti katika dakika za mwisho za mchezo huo, hali iliyompelekea kutoka nje.

“Following further investigation, Robin van Persie has a sprained knee, which will keep him out for around four to six weeks,Wishing you a speedy recovery, Robin.” alisema msemaji ya klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo atazikosa mechi za Champions League dhidi ya Bayern za April 1 na April 9 pamoja na baadhi mechi za ligi ya Premier League .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents