Michezo

Roger Federer avunja rekodi na kuweka ya kwake katika ulimwengu wa tennis

Mcheza tennis mwenye umri wa miaka 36, Roger Federer amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka mitano katika historia ya mchezo huo na kuvunja rekodi ya Andre Agassi aliyestaafu akiwa na umri wa miaka 33 mwaka 2003.

Federer ameandika historia hiyo baada ya hapo jana kushinda mchezo wake dhidi ya Robin Haase katika michuano ya dunia ya tennis ya ABN Amro inayo endelea huko Rotterdam.

Mchezaji huyo anayeshika nafasi ya pili katika viwango vya ubora duniani amesema kuwa anahitaji kuwa nafasi ya kwanza ambayo inashikiliwa na Rafael Nadal “Kushika nafasi ya kwanza nimoja ya lengo langu,”amesema Federa ambaye mchezo ujao anatarajia kukutana na Andreas Seppi aliyemshinda Muitalia Daniil Medvedev kwa seti 7-6(4) 4-6 6-3.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents