Burudani

Roma aeleza sababu za kuamua kutotumia mitandao ya kijamii kwa muda usiojulikana

Mitandao ya kijamii ndio sehemu ambayo mashabiki hupata nafasi ya kufahamu mambo yawahusuyo mastaa wanaowapenda kwa haraka zaidi, kitu ambacho mashabiki wa Roma wamekikosa kwa muda mrefu sasa.

roma new pic

Roma Mkatoliki amekuwa nje ya mitandao ya kijamii kwa zaidi ya miezi miwili sasa, ukiingia kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram post yake ya mwisho aliweka Octoba 24, 2015.

Ukimya wake wa kwenye mitandao hiyo uliibua uvumi kuwa huenda serikali imemfungia kutumia mitandao hiyo, kitu ambacho amekanusha sio kweli bali ni uamuzi binafsi alioufanya bila kushinikizwa na mtu.

Roma amesema ameamua kuchukua uamuzi wa kutotumia mitandao hiyo kwa muda usiojulikana, lakini hatajitoa kwasababu atahitaji kuitumia wakati wa kutangaza.

“Hii mitandao nimekuja kugundua kwa sisi Watanzania inachukua muda wetu mwingi sanja…kitu ambacho nimejaribu kuweza kuona ni kwamba hivi mimi si ninaweza kuishi bila kuwepo kwenye Instagram bila kupost chochote, basi nisijitoe niendelee kuwepo kwasababu kuna kazi yangu nitataka kuzitangaza baadae lakini kukaa tu kimya pasipo kupost.” Alisema Roma kwenye mahojiano na HZB TV.

Ameongeza kuwa licha ya kuwa hapost chochote kwenye mitandao lakini haijaathiri kazi zake kwa sababu anaendelea kupata interviews, shows na mambo mengine yahusuyo kazi yake ya muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents