Michezo

Ronaldo aanika saa yake ya gharama kabla ya kuivaa Manchester United leo, imejaa madini ya almasi

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo hapo jana usiku amekuwa gumzo kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kutinga na saa ya Jacob&Co Caviar Tourbillon range ambayo ni ya gharama kubwa na imejaa madini ya almasi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Cristiano Ronaldo showed off a diamond-encrusted watch at his press conference on Monday

Cristiano Ronaldo akiianika hadharani saa yake ya gharama iliyojaa madini ya almasi usiku wa jana katika mkutano na waandishi wa habari 

Mkutano huo uliyokuwa ukizungumzia mchezo wao wa UEFA Champions League utakao pigwa hii leo dhidi ya mashetani wekundu Manchester United, Ronaldo ameonekana akiwa amevalia saa hiyo ya gharama yenye rangi nyekundu.

Wachambuzi wanaeleza kuwa saa hiyo iyojaa zaidi ya vipande 424 vyeupe vya almasi inagharama ya pauni milioni 1.85.

Ronaldo ametuwa Manchester kwaajili ya mechi ya Champions League dhidi ya mabosi wake wa zamani United na atakuwa kwenye mstari wa mbele kuiyongoza timu yake ya sasa Juventus kuhakikisha inachomoza na ushindi ndani ya dimba la Old Trafford kwenye mchezo huo wa Group H.

Nyota huyo wa Ureno amekuwa balozi wa Jacob&Co tangu mwaka 2013 wakati akiwa Real Madrid na sasa ameamua kuonyesha moja kati ya bidhaa ghali kutoka kwenye kampuni hiyo wakati kwa mujibu wa Forbes calculations, mwana masumbwi, Floyd Mayweather anamiliki saa ya almasi yenye gharama ya pauni milioni 14 ya ‘billionaire diamond tourbillon’.

Kwenye kikao hicho na waandishi wa habari Ronaldo ameonekana akiwa ametulia licha ya siku za hivi karibuni kusumbuliwa na kesi ya kumbaka mrembo Kathryn Mayorga katika hotel ya Vegas mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents