Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Sakata la waliyokwama mapangoni lazua sura mpya, FIFA lawaalika vijana hao kombe la dunia

Mkasa wa watoto wa timu ya mpira ya wirld boys walionasa kwenye pango la chini kwa chini huko Thailand unazidi kuibua hisia duniani.

Rais wa FIFA Gianni Infantino ameialika timu hiyo kwenye fainali ya Kombe la duniani ikiwa wataokolewa salama wakati juhudi za kuwaokoa zinazidi kuendelea kwa kasi kubwa hii leo siku ya Jumatatu.

Wachezaji wanne kati ya 12 waliyokwama kwenye mapango nchini Thailand waokolewa (+Picha)

Infantino ameiyandikia barua rais wa soka wa Thailand (FA), Somyou Poompanmoung kwaajili ya mualiko wa watoto hao kushuhudia michuano endapo watatoka salama.

Image result for FIFA PRESIDENT, Infantino children have been stuck in the cave Thailand

“Tumekuwa tukifuatilia kwa ukaribu mkubwa habari hizi za uokoaji vijana 12 na kocha wao ambao wamenasa kwenye mapangono Kaskazini mwa Thailand huko Chiang Rai tangu kutokea kwa tukio hili Juni 23 mwaka huu 2018,” amesema Infantino.

Infantino ameongeza”Kwa niaba ya jumuiya ya soka ya kimataifa ningependa kuungana na wewe, familia na Wanathailand kwa ujumla  kwanyekipindi hiki kigumu. Tumaini letu, wachezaji na umoja wote kwa ujumla tunaimani punde watarudi salama, wenye afya na kujiamini.”

“Kama tunavyotarajia sote kwa pamoja kuwa watarejea salama na wenye afya kwenye familia zao waruhusuni wasafiri na FIFA tunawaalika kama wageni wetu kuushuhudia fainali ya michuano ya kombe la dunia 2018 jijini Moscow, ni tumaini langu tutaungana nao.”

Jumla ya wachezaji wanne wa timu ya vija waliyokwama kwenye mapango ya Chiang Rai nchini Thailand wamepata bahati ya kuokolewa hapo jana siku ya Jumapili kati ya wachezaji soka 12 waliyozama.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW