Burudani

Sanaipei Tande arejea kwa kishindo kwenye muziki

By  | 

Malkia muimbaji kutoka Kenya, Sanaipei Tande, alifanya vizuri kipindi cha nyuma akiwa member wa kundi la Sema ambalo pamoja na makundi mengine mawili, hapa nazungumzia Blue 3 kutoka Uganda na Wakilisha kutoka Tanzania ambayo pamoja yalijulikana kama The Cocacola Popstars, kitambo hicho, walifanya vizuri na wimbo “Leta Wimbo” licha ya kuwa na umri mdogo.

Kundi la Sema lilivunjwa baada ya muda mfupi mno na ndipo Sanaipei akaanza rasmi ‘solo career kwenye muziki na wimbo ‘Kwaheri’ aliofanya na Juakali ndio ulimtambulisha kama Sanaipei Tande. Aliendelea kufanya vizuri ila kuna kipindi akakosa kusikika kimuziki kwa kuwa alijihusisha na shughuli nyingine nje ya muziki wakati huo.

Sasa hivi hali hii imebadilika maana mrembo huyu mwenye sauti ya pekee amerudi tena kulijaza pengo aliloacha kwenye game. Tayari ameachia nyimbo mbili, “Amina” na “Simama Imara” ambazo tayari zinafanya vizuri redioni.

Nimepata nafasi ya kupiga story na huyu mdada, na alichosema kwa ufupi ni kwamba amepanga kufanya makubwa huu mwaka na tayari video ya wimbo wake kwa jina Amina ipo jikoni na amewataka mashabiki zake na yeyote ambaye ameipa nyimbo hiyo mapokezi makubwa wakae mkao wa kula kwa ajili ya video yake inayokuja soon.

Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amesema kuwa amejitahidi kuendelea kufanya audio kali na pia kufanya video aina hiyo hiyo. Kazi ni kwake sasa sisi macho kodo tukisubiri.

Na: Teddy Agwa
[email protected]
Facebook: teddybway

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments