Habari

Sean Kingston na mlinzi wake watuhumiwa kubaka ‘gang rape’

Mwimbaji kutoka Marekani mwenye asili ya Jamaica Sean Kingston na mlinzi wake wanatuhumiwa kumbaka (gang rape) msichana aliyekuwa amelewa katika chumba cha hoteli walioyifikia mwaka 2010.

Sean Kingston-BBC-016659

Kwa mujibu wa TMZ msichana huyo Carissa Capeloto (22) anayedaiwa kufanyiwa kitendo hicho na staa huyo , anadai kwamba alilazimishwa kufanya mapenzi na Sean, mlinzi wake pamoja na member mmoja wa bendi ya Sean katika hoteli ya Seattle July, 2010.

Capeloto amedai kuwa alikaribishwa na Kingston chumbani kwake katika hoteli hiyo kwaajili ya kusalimiana baada ya Sean kuperform katika concert ya Bieber, lakini baada ya kufika chumbani kwake alimkuta Kingston anamsubiri akiwa mtupu kitandani kwake.

Msichana huyo ameendelea kudai kuwa mlinzi wa Kingston alimnyanyua na kumuweka juu ya kifua cha Sean, na wote watatu wakaanza kumfanyia kitendo hicho (kumbaka) mpaka baadaye rafiki wa Capeloto alipoingia na kumuokoa.

Taarifa hiyo inaendelea kusema polisi waliitwa na Carissa alipelekwa hospitali na kutibiwa majeraha aliyoyapata kutokana na kubakwa.

Kutokana na hilo Capeloto anadai fidia ya dola million 5 kiwango cha chini kutokana na kwamba maisha yake yamevurungwa kwa kitendo kile.

Mashtaka ya jinai dhidi ya Kingston yalitupiliwa mbali mwaka 2010 baada ya maaskari kusema kuwa Capeloto hakuwa na vielelezo vya kutosha vya kuaminika kwaajili ya kufungua kesi.

Hata hivyo taarifa hiyo inaongeza kuwa sean Kingston amewsilisha nyaraka za kisheria kusisitiza kuwa walifanya mapenzi na msichana huyo kwa makubaliano asilimia mia.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents