Serena Williams aadabishwa na dada yake michuano ya Indian Wells

Mchezaji tennis raia wa Marekani mwanadada, Venus Williams amefanikiwa kumfunga mdogo wake, Serena Williams hatua ya raundi ya tatu ya michuano ya   Indian Wells na kuwa mwisho wa safari yake toka kurejea baada ya uzazi.

Mchezaji huyo aliyewahi kuwa namba moja katika viwango vya ubora duniani amepoteza mchezo huo kwa jumla ya seti 6-3 6-4.

Baada ya matokeo hayo, Serena Williams ambaye kwa mara ya mwisho amefungwa na dada yake, Venus mwaka 2017 katika michuano ya wazi ya Australia amesema kuwa bado safari yake ndefu na kamwe si yarahisi.

Baada ya ushindi huo Venus anafanikiwa kusonga mbele hadi raundi ya 16 ambapo atakabiliana na  Anastasija Sevastova ambaye amemfunga, Julia Goerges kwa seti  6-3 6-3.

Serena amerejea katika mchezo huo baada ya kutoka katika uzazi wa mwanawe, Alexis Olympia tarehe 1 ya mwezi Septemba mwaka 2017 wakati alipo mfunga, Venus kwa seti 6-4 6-4.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW