Michezo

Sergio Aguero aifungia ‘hat-trick’ Man City

Straika wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Leonel “Kun” Aguero ameifungia City mabao matatu ‘hat-trick’ katika mchezo wao wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Watford.

Mchezaji wa  Manchester City, Sergio Leonel “Kun” Aguero

Kun Aguero ameipatia mabao hayo katika ushindi waliyo upata wa mabao sita na hivyo kuifanya safu ya ushambuliaji ya City kuwa na jumla ya mabao 15 katika michezo  mitatu pekee.

Katika mabao hayo ya Aguero ya liyovunja mwiko kwa Watford kutofungwa katika Ligi msimu huu pia mchezaji mwingine wa City aliyefumania nyavu ni Gabriel Jesus aliongeza bao la tatu likiwa ni lake la tano msimu huu baada ya kufunga bao zuri kutokana na pasi iliopigwa na muargentina huyo.

Muargentina mwingine anayechezea nafasi ya mlinzi wa kati, Nicolas Otamendi alifunga kwa kutumia kichwa kutokana na kona iliopigwa na David Silva kabla ya Aguero kufunga bao lake la tatu, baada ya kuvamia ngome ya Watford akiwa pekee ndani ya eneo hatari.

Wakati karamu ya mabao ya City ikihitimishwa na  kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza, Raheem Shaquille Sterling  aliyefunga bao la sita kupitia mkwaju wa adhabu ya penati.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents