Michezo

Sharapova akiri kuzidiwa kiwango michuano ya China Open

Mchezaji tenis raia wa Urusi, Maria Yuryevna Sharapova ametolewa katika michuano ya wazi ya China ‘China Open’ baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Simona Halep katika hatua ya robo fainali.

Sharapova ambaye anashika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani ametolewa na Halep kwa jumla ya seti 6-2 6-2.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Maria Sharapova alikiri kuzidiwa kiwango na mromania huyo na kusema kuwa alikuwa bora zaidi yake.

Halep atakutana na mchezaji mwingine wa Urusi mwana dada Daria Kasatkina ambaye alipata ushindi wake kutoka kwa kumfunga Agnieszka Radwanska kwa seti 4-6 7-5 6-2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents