Michezo

Sikuwa na tatizo na Suarez, Messi amechukia-Kocha Barcelona

Ronald Koeman amesema kuwa Luis Suarez angeliweza kusalia Barcelona ili kum ‘prove wrong’ lakini badal yake ametimkia Atletico Madrid.

Striker huyo mwenye umri wa miaka 33, aliambiwa kuwa yeye sio haitajiki tena hasa kufuatia msimu baya wa 2019-20 na hatimaye kujiunga na Atletico paundi milioni 6 ikiwa ni chupuchupu atuwe Juventus.

Suarez amekuwa na miaka sita ya mafanikio ndani ya Nou Camp, akishinda Champions League na mataji manne ya LaLiga huku akiwa na mwanzo mzuri kwa waajiri wake wa sasa ambapo tayari ameshaweka kambani magoli mawili mpaka sasa ndani ya Atletico.

Koeman amekuwa akisisitiza Suarez angeendelea kubaki kama yeye alivyokuwa anatamani ”Kwa kesi ya Suarez, ili kuwa ngumu sana kwake kuanza kucheza na nilimfanya ajuwe hilo. Alikuja kujua itakuwa ngumu lakini sikuwa na tatizo naye kabisa,” Koeman ameiyambia NOS.

”Alikuwa anafanya mazoezi kawaida tu, amefundishwa vizuri, baade akaamua kuchukua maamuzi ya kuondoka na nikamwambia kama hukuondoka kwa sababu zozote zile basi wewe ni mmoja miongoni mwa kundi na utanithibitishia kuwa nilikuwa nimekosea kukuondoa,” amesema kocha huyo huku akiongeza angeweza kukaa ndiyo

”Sina tatizo na Luis, lakini klabu ilihitaji kufanya mabadiliko makubwa ndani ya klabu hata wewe unaweza kuona ndani ya timu.”

”Ansu Fati ana miaka 17, tuna Pedri, 17, Ronald Araujo miaka 21. Trincao, 20, tumemchukua Sergino Dest, ambaye naye ana miaka 19. Wachezaji hawa wote ni wapo kwaajili ya siku zijazo.”

Lionel Messi alikuwa akikosoa sana jinsi Barcelona ilivyoshughulikia kuondoka kwa Suarez na Koeman aligusia kwamba amezungumza naye juu ya jambo hilo.

Nilimwambia pia MessiĀ  kuwa nafahamu umejisikia vibaya na kukata tamaa ”Unafikiri kama kitendo cha haibu kwa namna alivyoodoka lakini hilo lilikuwa chaguo la klabu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents